Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

BRAND NEW RELEASE #TWAJIACHIA BY MZUNGU KICHAA FT. MALFRED


Dear friends and supporters, 
 I am very please to be able to share a brand new song and video with you. Twajiachia was recorded at Tao Studio in Hamburg, together with German producer Flo Bauer during the Mzungu Kichaa and Malfred tour at the end of 2014. 
Their Tanzanian backing band Bongo Beat also joined them for the recording session. 
All musicians are featured in the music video, which was directed and shot on location in Hamburg by Zeki Oguz Teoman. 
The video represents the journey of 6 musicians from Tanzania, who during their tour, do a quick visit for a one day studio session, and record from the heart and from the fingertips.
Twajiachia literally means ‘we are letting go’ but in slang it would translate more towards ‘we are having fun’. The chorus ends with the line ‘ngoma likipigwa tuna pata raha tele’ which means ‘when the drum beats, we are filled with joy’. ‘At times we all face hardships and music can be an important tool to help bring back the joy and purpose in life. Twajiachia is meant to do exactly this!’ – Mzungu Kichaa. 
 The song is an example of the globalization of urban club music: an upbeat fusion between European electronic sounds, Bongo Flava and Jamaican dancehall. 
 Please tag @mzungukichaa,
 @malfred and hashtag #twajiachia when posting your comments or links to social media so that we can repost and share your thoughts and comments with our followers.
Espen Sorensen
 - Mzungu Kichaa

HAWA NI WASANII AMBAO MPAKA SASA WAMESHATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA HUU

Wasanii wa Tanzania, Safari hii wameamua kugombea Ubunge katika maeneo mbalimbali. Hawa ni baadhi ya wasanii walio amua kugombea mwaka huu 2015
                                                                      Profesa Jay, Mikumi-
Nimeamua kugombea jimbo la Mikumi kwa kuwa ni nyumbani. Wazazi wangu waliishi hapa kwa muda mrefu lakini pia nimekuwa nikiimba siasa sana na sasa nimeona huu ni muda wa kufanya yale niliyokuwa nikiimba kuuhusiana na maendeleo ya taifa.”
                                                                  Dude, Tabora Mjini- 
Nimeanza kufanya maandalizi ya kugombea ubunge nyumbani kwetu Tabora mjini, niko tayari kuchuana na yeyote na sasa niko kwenye maandalizi ikiwemo kuwa karibu na wananchi kwani wananikubali, hivyo nitahakikisha ninapata ushindi.
                                                                         JB, Kinondoni-
Nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda mwafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii.”
                                                                Soggy Doggy, Segerea
Soggy Doggy ametangaza kugombea ubunge wa jimbo hilo, jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chadema. Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa Makongoro Mahanga (CCM).
                                                                  Steve Nyerere, Kinondoni
Ukiona chereko chereko ujue mambo yameiva, nitagombea ubunge 2015. Nimejipanga na ninaweza kufanya hivyo, nipo vizuri sana.” Jimbo hilo la Kinondoni liko chini ya Mhe. Idd Azzan (CCM).

                                                           Afande Sele, Morogoro Mjini
Niliumizwa baada ya kusikia kuwa eti katiba ya chama cha Chadema inasema kuwa mwanachama anayekwenda mahakamani kudai haki yake anakuwa amejivua uanachama wake. Kwa chama kama Chadema sikuamini kama kingekuwa na sheria kandamizi kama hiyo ya kuwazuia wanachama wake kwenda mahakamani, ndio maana nimeamua nijiunge na chama kingine ambacho kitakuwa kinamuweka huru mwanachama kudai haki zake.” Jimbo la Morogoro Mjini kwa sasa lipo chini ya Mohamed Aziz Abood (CCM).
                                                                 Dokii, Kilosa Morogoro
Mimi ni msanii pekee naweza kusema ndiyo nimetumika sana kwenye jamii kuliko wasanii wote, kwenye kuelimisha jamii najitolea hata kipindi kile cha madereva wa bodaboda mpaka wakanipa Ubalozi nilikua natetea haki zao, pia nataka kuonyesha kwamba wanawake tunaweza.”
Jimbo la Kilosa liko chini ya Mustafa Mkulo (CCM) ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha kabla ya kujiuzulu.
                                                          King Majuto, Tanga Mjini
Mujibu wa maneno yake anasema lengo kubwa ni kutaka kuinua uchumi wa Tanga pamoja na kutetea haki za wananchi pamoja na rasilimali za Mkoa huo. “Nitarudisha Tanga ya zamani ambayo ilikuwa ikisifika sehemu mbalimbali kutokana na rasilimali zilizopo ambazo kwa sasa zimeshindwa kusimamiwa na kuwanufaisha watu wa Tanga.” alisema Majuto ambaye atakua akichuana na mbunge wa sasa wa Tanga Mjini, Omari Nundu (CCM).
                                                                      Shilole, Igunga
Baada ya Dalali Kafumu anayefuata ni mimi, mimi nadhani napenda jimbo langu na nawapenda wakazi wangu wa Igunga wananiona tangu nakua mpaka sasa hivi, kwa hiyo wanafurahi. Sasa wananiambia ‘sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa na hivyo wananipa changamoto,” alisema msanii huyo.
Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza nitatetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani akinamama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo nitawatafutia kazi na nitajenga chuo cha muziki".
                                                                      Kalapina, Kinondoni
Kwanza sasa hivi anaitwa mbunge wa Kinondoni, hivyo nitagombea uchaguzi ujao. “Kuna mambo mengi ambayo nimepanga kuifanyia Kinondoni,’’ anasema kalapina.
                                                                  Mrisho Mpoto, Ubungo
“ Nataka kurudisha heshima, utamaduni na maisha bora kwa watu wa Ubungo.” Jimbo la Ubungo kwa sasa liko chini ya John Mnyika (Chadema).
                                                                           Kingwendu
Mwigizaji Kingwendu, anasema anajiandaa kugombea ubunge mwaka huu 2015.Hata hivyo, Kingwendu hakuweka bayana atagombea jimbo gani wala kupitia chama gani, isipokuwa zaidi anasema kuwa chama ambacho kinapendwa na Watanzania wengi ndicho atatumia tiketi yake.
Kingwendu anasema, “Ninajiandaa kugombea ubunge 2015 kupitia chama ninachoona kinapendwa na Watanzania wengi kwenye jimbo ambalo nitalitaja hapo baadaye wakati utakapofika, bado ninafanya mazungumzo na washauri wangu wa karibu kuhusiana na suala hilo, nadhani nitaliweka wazi muda ukifika.”
                                                                   Juma Chikoka, Ilala.
Msanii wa sanaa ya maigizo na filamu, Chikoka maarufu kwa Chopa Mchopanga au Mzee wa Halmashauri ya Kichwa, Mwaka 2010 aliwahi kuchukua fomu na kujitosa kwenye siasa kwa kugombea ubunge wa Jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini alishindwa kwenye kura za maoni za chama hicho na mbunge wa sasa wa jimbo hilo Mussa Zungu.
Mwaka huu wa 2015, amepanga kujitosa tena na safari hii anasema kuwa kinachomsukuma hadi kuamua kugombea tena ni kutaka kuwawakilisha vijana wenzake katika ngazi ya juu ya uongozi na kupambana na uhaba wa ajira kwa vijana.
Anasema kuwa yeye ni mzoefu katika siasa, kwani alishawahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni, mhamasishaji wa vijana, pia ni mmoja kati ya waanzilishi wa matawi ya CCM nchini India

JB AKANUSHA KUGOMBEA UBUNGE KINONDONI

Staa mkubwa wa Bongo Movies, Jacob Stephen ‘JB’ amekanausha taarifa za kutaka kugombea ubunge jimbo la kinondoni ambazo zimekuwa zikienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
JB ameeleza kuwa japo watu mbali mbali wamekuwa wakimfuata na kumtaka agombee yeye amekuwa akiwashukuru na kuwaeleza kuwa anaipenda sana kazi yake ya uigizaji.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Instagram aliyaeleza hayo akiwa anatolea ufafanuzi kile ‘mrekebishatabia’ alichokiandika kwenye mtandao huo.
@mrekebishatabia,  Na mimi nimezisikia habari hizo eti nataka kugombea k,ndoni. si za kweli ingawa kuna kundi kubwa lilinifata na kunishawishi nigombee lakini niliwajibu nashukuru kwa kunifikiria lakini nafurahia kazi ya uigizaji kuliko kazi nyingine...
Awali ‘mrekebishatabia’ alitoa orodha ya wasanii wanasemekana kuwania ubunge ambapo aliandika;
Kwa mujibu wa jamiiforums hawa ndo wasanii wanaowania kugombea Ubunge 2015
1. Prof Jay- Mikumi
2. Dude- Tabora Mjini
3. JB- Kinondoni
4. Soggy doggy- Segerea
5. Steve Nyerere - Kinondoni
6. Afande Sele- Morogoro Mjini
7. Dokii- Kilosa Morogoro
8. King majuto- Tanga Mjini
9. Shilole- Igunga
10. Kalapina- Kinondoni
11. Baba Levo (haijawekwa wazi)
12. Juma chikoka-Ilala
13. Kingwendu- hajaweka wazi jimbo
14. Wema sepetu- Singida 
Mwingine nani??? Mambo yanaelekea yatachanganya hapo baadae. Kila la heri wasanii wote.

LUCY KOMBA: NAMIMI NAKUJA KUGOMBEA UBUNGE SONGEA

Staa wa Bongo Movies, Lucy Komba ambaye kwa sasa anaishi ughaibuni ameonesha nia yake ya kurudi ya kuja kuwania ubunge. Lucy ameyaseme hayo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao picha wa instagram ambapo alianza kwa kuwapongeza wasanii wenzake wote walioamua kujikita kwenye siasa.
“Msiseme wanawake tu semeni pia na wasanii tunaweza, hongereni wote wasanii mlioamua kujikita kwenye siasa na mimi nakuja huko kuchukua ubunge wa kwetu Songea”- Lucy ameandika.
Kila la kheri Lucy

UJUMBE: KAMA WEWE NI KIJANA, MONALISA ANA HILI KWA AJILI YAKO

"Kijana,ichunge sana LEO yako.Hujui kESHO utafanya nini au utakuwa nani.KESHO itakapofika watu watakuhukumu kwa JANA yako ambayo ni LEO.Chunga sana LEO yako ndio inayokutengenezea KESHO yako." YVONNE CHERRIE
Roho yangu imenisukuma tu kukuandikia ujumbe huu..pengine nitaokoa LEO ya mtu fulani..Kila la kheri 
Monalisa on Instagram

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI TAREHE 21/06/2015













Haya ndio magazeti ya leo tarehe 21/6/2015, usikose nakala yako

TFF WA MFUKUZA KAZI KOCHA WA TAIFA STARS

RELEASE NO. 102

TAREHE 20 JUNI, 2015

KAMATI YA UTENDAJI YASITISHA AJIRA YA NOOIJ
Kamati ya utendaji ya Shirikishi la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Katika kikao chake cha leo pamoja na mambo mengine ilipitia mwenendo wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mchezo kati ya Tanzania na Uganda, kama sehemu ya tathmin ya mwenendo wa timu.

Kamati ya utendaji kwa kauli moja imeamua yafuatayo:

1.Ajira ya Kocha Mkuu Maart Nooij inasitishwa mara moja kuanzia  tarehe 21/June/2015.
ΔΆ
2.Benchi lote la ufundi la Taifa stars limevunjwa kuanzia tarehe 21/06/2015.

3.Uongozi wa TFF utatangaza punde benchi jipya la ufundi la timu ya Taifa.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

-- 
Best Regards,

Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
T: +255 22-2861815  I F: +255 22-2861815  I C: +255 713 455970 
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W:
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top