Kamati ya Miss Universe Tanzania imemteua mshindi wa pili wa Miss Universe 2014, Nale Boniface kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe yatakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwa kwanza 2015 Miami, Marekani.
Hatua hii imechukuliwa baada ya mshindi husika Miss Universe Tanzania
2014, Carolyne Bernard kupata ajali na kuvunjika kidole chake cha
mguu. Ripoti ya daktari imeonyesha kuwa kupona kwake kutachukua mwezi
mmoja wakati mrembo anatakiwa awe mashindanoni baada ya siku kumi
kuanzia sasa. Isitoshe awapo mashindanoni mrembo atapaswa kuvaa viatu
virefu (High heels) wakati wote ambapo haishauriwi kiafya kutokana na
tatizo lake.
Hivyo kutokana na hali hii, Nale Boniface ambaye alishika nafasi ya pili
na aliwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth ndiye
atakayekwenda kuiwakilisha nchi badala yake kama mkataba unavyoainisha
na hivyo atakuwa Miss Universe Tanzania 2014.
Kamati inasikitishwa na kuumia kwa Carolyne na inaahidi kuendelea
kuwa nae bega kwa bega katika matibabu yake kwani bado yupo chini ya
mkataba wa Miss Universe Tanzania kwa mwaka mzima.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania mwaka huu yalifanyika tarehe 31
mwezi wa Kumi na yalidhaminiwa na Insignia, Golden Tulip, Compass
Communications, AzH Photography, Adams Digicom, Opulence, Seif Kabelele
Blog , Missie Popular blog, Urban Rose Hotel, na New York Film Academy.