Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

NEWS ALERTS: OKWI AREJEA MSIMBAZI

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mganda Emmanuel Okwi, ambaye wiki iliyopita alikwenda kwao Uganda kufunga ndoa amerejea Dar es Salaam na kujiunga na Kambi ya timu yao, Zanzibar.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Okwi alisema yuko fiti anakwenda kuungana na wachezaji wenzie, anatumaini kufanya mambo makubwa katika mchezo huo raundi ya nane Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Okwi alikwenda kwao Uganda ambapo Jumamosi iliyopita ambapo alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Nakalega Florence kabla ya kurejea nchini juzi usiku na jana mchana alikwenda Zanzibar kujiunga na wenzake.
Licha ya kuwa timu hiyo leo inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kabla ya mchezo wao dhidi ya Kagera, Okwi ambaye alikuwa nahodha katika mechi ya Nani Mtani Jembe Desemba 13, ambapo aling’ara na kuiwezesha kushinda mabao 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi Yanga, alisema ameona ni muhimu kwenda kuungana na wachezaji wenzie kambini.
Akizungumza na Jambo Leo Dar es Salaam jana, Okwi alisema anaamini kuwa timu yao itafanya makubwa kuanzia kwenye mchezo wao dhidi ya Kagera.
“Nimerejea na nguvu mpya na naamini kuwa Simba hii itakuwa ni tofauti na ile iliyopita ambapo tutaanza na ushindi katika mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar,” alisema.
Simba imeweka kambi ya wiki moja visiwani humo kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara, ambapo wanatarajiwa kujerea Dar es salaam kesho asubuhi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Kagera utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Simba iko katika nafasi ya saba kwenye msiamo wa Ligi Kuu ya Tanzania ikiwa na pointi tisa ilizopata katika mechi saba. Imeshinda mechi moja kutoka sare sita, haijapoteza mechi, imefunga mabao saba na kufungwa sita.
Mtibwa Sugar inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 15, inafuatiwa na Yanga na Azam ambazo kila moja ina pointi 13 huku zikifuatiwa na Coastal Union (11), Ruvu Shooting na Kagera Sugar (10).
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top