Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

YANGA KUPITIA MIKATABA UPYA, YAJITOA MAPINDUZI CUP

KLABU ya Yanga imetoa mikakati yake mipya ambapo itapitia upya mikataba yake, kuzalisha wachezaji na kuthibitisha kushiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoanza kutimua vumbi Januari mosi mwakani, visiwani Zanzibar.
Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Jonas Tibohora, alisema Dar es Salaam kuwa klabu yao itashiriki michuano hiyo kwa kuwa itaisaidia timu yao kupata mazoezi.
Mwaka jana Yanga ilipewa nafasi ya kushiriki mashindano hayo lakini ilijitoa katika dakika za mwisho, kitu kilicholalamikiwa na baadhi ya wanachama, mashabiki wao na wadau wa soka.
Tibohora alisema kupitia michuano hiyo wataweza kukijenga zaidi kikosi chao ambacho kinashiriki Michuano ya Kombe la Shirikisho ambayo katika mchezo wa awali imepangwa kuchuana na timu ya Jeshi la Botswana (BDF).
Alisema kuwa licha ya kuwa bado hajaona barua ya mwaliko, akiipata moja kwa moja watathibitisha ushindi wao kwa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), na kupeleka timu.
“Sisi tunahitaji mechi tofauti sio za Ligi Kuu tu, ni pamoja na mechi za michuano hiyo ambazo zitashirikisha timu kutoka Zanzibar na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na Kati, tunashiriki kukijenga zaidi kikosi chetu,” alisema Tibohora.
Alisema akizungumzia mkakati huo, alisema wamejipanga kuanzisha Kituo kitakachokuwa na timu tatu za vijana chini ya umri wa miaka 15, 17 na 20 ambao watakuwa wakipandishwa kwenye timu kubwa.
Tibohora alisema wamejipanga kuhakikisha wanaachana na tabia ya kununua wachezaji wengi, ambapo klabu yao itakuwea kama ilivyokuwa zamani.
Alisema licha ya klabu yao kujipanga kuwa klabu ya mfano kwa kuibua vipaji kama ilivyokuwa zamani, itahakikisha inajiendesha kupitia nembo ya klabu hiyo.
Pia Tibohora, Yanga imeanza kupitia mikataba yote ya klabu hiyo, ikiwa ni pamoja na mkataba wa Azam TV, ambao klabu hiyo iliugomea na kutochukua fedha za udhamini wao wa matangazo ya televisheni.
Tibohora alisema kuwa haiwezi kuingia mkataba bila ya kuangalia maslahi ya klabu hiyo kubwa hapa nchini.
“Natambua kila mtu anafahamu ukubwa wa klabu yetu, hivyo ni lazima tuangalie mikataba yote sio tunaingia mkataba na baadhi ya timu ambazo bado hazijafikia ukubwa wa timu yetu,”alisema.
Yanga imewaajiri watendaji wapya wanaongozwa na Jonas Tibohora kama Katibu Mkuu, huku Ofisa Habari akiwa Jerry Muro na Ofisa Masoko akiwa Omary Kaya .

Source: Jambo leo
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top