Sanaa ya uchekeshaji ni moja ya kazi ngumu ambazo wachache hufikiria kama kazi ya "lele mama"! hakuna, hii ni kazi ngumu sana. Akiongea na mtandao huu, mchekeshaji anayetumia mtindo wa kipekee hapa Bongo, ambaye kazi zake zitaanza kuonekana "Live" muda si mrefu, Mr. Matandiko ameonekana kuiongelea sanaa hii ya ufutuhi kwa mapana sana.
Pia ameelezea kuwa, mtindo anaotumia yeye ni moja ya mitindo migumu sana ila ni rahisi mtu yeyote kukuelewa.
"Unajua huu mtindo wa mime comedy ni mtindo mgumu lakini mtu wa lugha yoyote atakuelewa, hata kama atakuwa ni mzungu au mchina, Mjapani au kutokea Amerika, lazima aelewe tu kuwa unamaanisha kitu gani, sema tu ni ngumu kuitunga hadi iwe movie kamili kabisa. Katika movie zangu nitafahamika kwa jina la Mr. Matandiko", alisisitiza.
Fuata hiyo link uweze kuongea naye Live.