MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa), kwa mara ya tatu baada ya kupata mafanikio makubwa akiwa na timu yake ya Santiago Bernabeu kwa mwaka 2014 .
Ronaldo ambaye ni Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno ametwaa tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo katika mwaka ambao amevunja rekodi ya ufungaji mabao katika msimu mmoja kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa kwa kupachika wavuni mabao 17, ambapo timu yake ilitwaa taji hilo kwa mara ya 10 .
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United katika msimu uliopita aligawana tuzo ya Kiatu cha Dhahabu Ulaya na Luis Suarez kwa kufunga mabao 31 katika La Liga katika msimu uliopita licha ya kukumbwa na umajeruhi wakati fulani.
Licha ya kuwa Ronaldo hakuweza kuisaidia timu yake katika hatua ya makundi, mabao 61 aliyofunga katika klabu yake na nchi yake 2014 yalimsaidia kupata tuzo hiyo yenye hadhi kubwa kwa mchezo binafsi kwa mara ya pili mfululizo.
Akizungumza wakati wa kupokea tuzo hiyo Ronaldo alisema:” Ni mwaka ambao hauwezi kusahaulika, kutwaa tuzo hii ni kitu cha kipekee. Ninachoweza kusema ni kuwa ninataka kuendelea kama nilivyo, kujaribu kwenda kutwaa makombe mengi zaidi.
“Ninataka kusema kwa kireno, Sikuwahi kufikiria kutwaa tuzo hii kwa mara ya tatu, bila shaka ni kitu ambacho kila wakati kimekuwa na mimi.
“Ninataka kuwa mmoja wa wachezaji mahiri wa wakati wote, hii inataka jitihada nyingi, ningependa kuwashukuru wote.”
Ronaldo alitwaa ushindi kwa kupata asilimia 37.66 ya kura, huku nyota wa Barcelona, Lionel Messi akishika nafasi ya pili na mlinda mlango wa Bayern Munich na Ujerumani Manuel Neuer akishika nafasi ya tatu.
Messi amekosa tuzo hiyo baada ya kuwa na msimu mgumu katika klabu yake ambayo haikutwaa kombe lolote msimu uliopita ambapo Barca ilipoteza matumaini ya kutwaa ubingwa wa La Liga katika siku ya mwisho dhidi ya Atletico Madrid kushindwa katika Ligi ya Mabingwa na Copa del Rey.
Nahodha huyo wa Argentina alitajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano ya Kombe la Dunia 2014 baada ya kufunga mabao manne na kufungwa katika fainali dhidi ya Ujerumani ambayo langoni alikuwepo Neuer.
Licha ya kuvunja rekodi ya Raul ya ufungaji mabao mengi katika Ligi ya Mabingwa na kuwa mfungaji mabao mengi za Ronaldo.
Kwa upande wa, Neuer hakuweza kupata zawadi, alibaki kuwa mshindi wa Tatu akipata asilimia 15.72 ya kura.
Neuer angeshinda tuzo hiyo angekuwa kipa wa pili nyuma
, Lev Yashin aliyewahi kuitwaa.
, Lev Yashin aliyewahi kuitwaa.
Mlinda Mlango wa timu ya wanawake ya Bayern Munich, Nadine Kessler alitwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kike wa Mwaka, huku Kocha wa Ujerumani Joachim Low na Ralf Kellerman wa timu ya wanawake ya Wolfsburg wakishinda katika kategoria ya Kocha Bora wa Mwaka.
James Rodriguez alishinda tuzo ya Mfungaji bao Bora la Mwaka ‘Puskas award’ kwa bao alilofunga kwenye michuano ya Kombe la Dunia akiichezea Colombia dhidi Uruguay katika hatua ya mtoano ya timu 16.
