Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

“MAMA KANUMBA ANASTAHILI FARAJA SIO KASHFA”, LUCY KOMBA

Lucy Komba : Mama Kanumba Anastahili Faraja Sio Kashfa
Staa wa Bongo Movies ambae kwa sasa anaishi ughaibuni, Lucy Komba amewatolea uvivu mashabaki wanaojifanya kumpenda Kanumba  huku wanamkashifu mama yake.
“Jamani mimi nimeguswa sana au kuumia na jinsi ambavyo watu wanatoa maoni na kumsema vibaya huyu mama. Mama kanumba hakustahili maneno ya kashfa alistahili maneno ya hekima na kuendelea kumfariji, watu wengi wamekuwa wakisema hakuna kama Kanumba hakuna wa kuweza kushika nafasi ya Kanumba na wengi kudai kummisi na kudai wanaendelea kumkumbukaa lakini mjue Kanumba hakujileta mwenyewe duniani marehemu Kanumba alizaliwa na binadamu ambaye ni mama yake na mama huyo ndo leo anapokea maneno ya kejeli na kashfa kutoka kwa wapenzi wa Kanumba mara arudi kijijini akalime nk.
Huyu mama aliishi mjini hata kabla mwanae hajawa maarufu na ni yeye aliyekuwa anajinyima kumsomesha mwanae na mpaka kufikia anakuwa super star, tusiwe wanafiki.
Huyu mama hajaomba msaada kwa mtu yeyote kama laiti Marehemu anaona au kusikia mama yake anakashifiwa na watu ambao wengine walizimia makaburini kumlilia Kanumba basi angeweza kuwachapa vibao wote. Huyu mama anastahili kuheshimiwa kama alivyokuwa akiheshimiwa mwanae.
Anauchungu na ataendelea kuwa na uchungu kwa mwanae siku zote za maisha yake anastahili faraja na siyo kashfa”- Lucy aliandika kwenye ukurasa wake mtandaoni.
Hivi juzi kati mama Kanumba alinukuliwa na gazeti moja la udaku akitoa lawama zake wa staa Elizabert Michael ‘Lulu’kuwa sasa hivi amemtenga hawapo kama zamani hapo ndipo baadhi ya mashabiki wakaanza kumshambulia mama huyu.
Picha: Mama Kanumba akiwa na Lulu zamani
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top