Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

HABARI NJEMA: YANGA SC YAWAOTEA WAARABU, SHUHUDIA MTANANGE HAPA...

 
Wachezaji wa Yanga wakishangilia goli.
 KOCHA wa Yanga, Hans van Der Pluijm, jeuri sana, kwani amefanya mazoezi mara mbili na kikosi chake kisha akawasisitizia wachezaji wake kwamba, wote lazima wakabe kisawasawa kuanzia mwanzo hadi mwisho katika mchezo wao dhidi ya Etoile du Sahel leo Jumamosi usiku. 

Yanga ipo jijini hapa tangu juzi kujiandaa na mchezo wake wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Etoile du Sahel utakaochezwa kwenye Uwanja wa Olympique uliopo kwenye mji mdogo wa Sousse.Timu hiyo ambayo tayari imeshatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, ilitoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya awali na leo inahitaji ushindi wowote au sare ya kuanzia mabao 2-2 ili isonge mbele. 

Katika mazoezi ya juzi jioni na jana usiku, Pluijm alionekana kutumia muda mwingi akiwaelekeza wachezaji wake kucheza kwa kuzuia muda wote bila kukwaruzana na adui.“Hakuna kitu kitakachotuwezesha kufanya vizuri kama kukaba, tutakaba kuanzia mwanzo hadi mwisho wa mchezo na haijalishi kama tutakuwa tunaongoza au tumetanguliwa kufungwa.
 “Wachezaji wangu wote wapo vizuri kwa mchezo huu, kidogo hali ya hewa inatuchanganya kama unavyoona kwani mchana kuna joto lakini usiku kuna baridi kali, hivyo nimewaandaa wachezaji wangu kushinda na sitaki hali ya hewa iwe kikwazo kwetu,” alisema Pluijm. 

Kuhusu kukosekana kwa Haruna Niyonzima ambaye ameachwa jijini Dar es Salaam kwa kuwa ni mgonjwa, Pluijm alisema: “Kweli kumkosa Haruna ni tatizo lakini nikwambie kitu, hawa wachezaji unaowaona wote wana uwezo wa kucheza na kuipigania Yanga, tutapambana.”
 Katika mazoezi hayo, Pluijm alionekana akiwasisitizia jinsi ya kukaba viungo Salum Telela na Said Juma Makapu ambao wanasifika kwa umakini wa kuzuia katika kiungo. 

YAKWEPA HUJUMA
Kama ilivyokuwa inatarajiwa, Yanga ilipowasili Tunisia katika mji mkuu wa Tunis, ilitumia saa tatu kukamilisha taratibu za uhamiaji lakini ikakumbana na kisanga cha kupewa basi dogo chakavu ili walitumie kwenda Sahel ambako ni mwendo wa saa mbili barabarani.“Hatukulitumia basi lile bovu, badala yake tumetumia letu tulilolikodi kama unavyoona, hili walilotupa tumewapa waandishi wa habari na maofisa wengine walitumie,” alisema mmoja wa maofisa wa Yanga.
 

Yanga ilikumbana na tatizo la kufanya mazoezi kwenye uwanja wenye taa hafifu juzi Alhamisi huku wenyeji wao wakishindwa kutoa sababu za kufanya hivyo.Aidha maofisa wa Yanga wamejipanga kuweka ulinzi katika vyumba vya kubadilishia nguo kwenye Uwanja wa Olympique watakapochezea mechi hiyo ili kukwepa hujuma ya kupuliziwa dawa za kupunguza nguvu. 

Katika Hoteli ya El Mouradi Palm Marina walikofikia Yanga kwenye mji mdogo wa Sousse, Sahel, maofisa wa timu hiyo wapo makini wakifuatilia kila kitu kinachofanywa na wafanyakazi wake ili kukwepa hujuma zozote.
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top