Imelda mtema
MZAZI mwenzake Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’, Faiza Ally hivi karibuni alizua gumzo baada ya kutinga kwenye shoo ya Zari White Party pande za Mlimani City jijini Dar akiwa ametinga shati pekee huku upande wa chini wa mwili wake akiwa hajavaa chochote.

Akizungumza na mwanahabari wetu, Faiza ambaye huko nyuma alishawahi kuvaa ‘Pampers’ ukumbini katika sherehe yake ya kuzaliwa, alisema kama ilivyokuwa awali, haoni tatizo lolote kutinga shati hilo pekee mwilini.
“Unajua binadamu bwana nilivyovaa Pampers wamechonga sana sasa nilivyotinga shati bado watu wanachonga, sasa lipi jema na vazi hili nililovaa nililifurahia sana kutoka ndani ya moyo wangu,” alisema Faiza.