Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

SALMAN KHAN, KUMGONGA NA KUMUUA MTU KWA GARI, JELA MIAKA 5


 Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa mjini Mumbai.
 Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo.
Salman Khan akitoka mahakamani na mama yake Sushila Charak 
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anayepaswa kulaumiwa lakini 


mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo. Kwa mujibu wa jaji wa mahakama hiyo mwigizaji huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

HABARI NA BBC SWAHILI
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top