
Nay wa Mitego bado ana hamu ya kuiongeza zaidi familia yake.
Rapper huyo mwenye watoto watatu amesema ana hamu ya kupata mtoto wa nne.
“Suala la uzazi wa mpango nalizingatia sana. Sasa hivi nina watoto watatu bado mmoja tu. Unajua hutakiwi uzae watoto wengi halafu waje kushangaa tu bila msaada,” amesema Nay.
- “Mimi hawa wanne watasoma vizuri kwa sababu tayari toka naanza maisha nilipanga kuja kuwa na watoto wanne.”