LONDON, England
MABINGWA watetezi wa Kombe la FA, timu ya Arsenal, imefuzu raundi ya nne ya kombe hilo baada ya kuichapa Hull City mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini hapa.
Mbali na mechi hiyo, vinara wa Ligi Kuu ya England, Chelsea nayo imeichapa Watford mabao 3-0, Manchester United ikaifunga Yeovil mabao 2-0 na Manchester City ikaichapa Sheffield Wednsday 2-1.
Katika mechi ya Arsenal, ilikuwa na ushindani kutokana na timu hizo kuwa zilicheza fainali ya kombe hilo mwaka jana na Arsenal ikaibuka na ushindi.
Kutokana na hali hiyo, wachezaji walikamiani kwa kucheza wakitumia nguvu ambapo mabao ya Arsenal yalifungwa na nahodha, Per Mertesacker kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Alexis Sanchez kipindi cha kwanza na kipindi cha pili Sanchez alifunga bao la ushindi.
Arsenal ilionekana kutawala mchezo kwa kiasi kikubwa na kasi si jitihada za kipa, Harper kuwa makini golini, timu hiyo ingefunga mabao mengi zaidi.
Katika mechi ya Chelsea, mabao yao yalifungwa na William, Loic Remy na Kurt Zouma na kuifanya timu hiyo pia kufuzu hatua inayofuata.
Man City ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Etihad, ilijikuta ikiibuka na ushindi huo kwa mabao yaliyofungwa na James Milner na lile la kufutia machozi likifungwa na Atdhe Nuhiu.
Majirani wao wa jiji la Manchester, Manchester United nayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yeovil ambapo mabao yao yalifungwa na Andy Herrera na Angel di Maria.
Herrera alifunga bao la kwanza la aina yake akiwa nje ya eneo la hatari kwa shuti lililomshinda kudaka kipa, Steer.
Katika mchezo huo, aliyekuwa kocha wao, Sir Alex Ferguson alitua uwanjani hapo kwa helkopta.
Matokeo ya mechi zingine za kombe hilo ni kama ifuatavyo;
Dover 0 – 4 Crystal Palace
QPR 0 – 3 Sheff Utd
Sunderland 1 – 0 Leeds
Aston Villa 1 – 0 Blackpool
Southampton 1 – 1 Ipswich
Stoke 3-1 Wrexham
Dover 0 – 4 Crystal Palace
QPR 0 – 3 Sheff Utd
Sunderland 1 – 0 Leeds
Aston Villa 1 – 0 Blackpool
Southampton 1 – 1 Ipswich
Stoke 3-1 Wrexham
