Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

ROBBEN AMWAMINIA SCHWEINSTEIGER

BERLIN, Ujerumani
WINGA Arjen Robben anatumaini kuwa mchezaji mwenzie wa Bayern Munich, Bastian Schweinsteiger atarejesha kiwango chake baada ya kuanza mwaka mpya.
Nahodha msaidizi Schweinsteiger alirejea uwanjani Novemba baada ya kukaa nje muda mrefu akiunguza goti, amecheza mechi nane za mashindano yote katika kikosi cha mabingwa watetezi wa Bundesliga .
Kiungo huyo alifunga bao lake za kwanza katika mchezo ambao timu yake ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Mainz uliopigwa katikati ya Desemba.
Robben anataka Schweinsteiger kurejesha kiwango chake wakati wakati ambapo timu ya Bavarians inataka kutwaa makombe matatu ikiwa chini ya Pep Guardiola.
“Basti ni mmoja wa manahodha wetu, ndivyo ilivyo,” Robben aliiambia tovuti ya Bayern.
Alisema mchezaji huyo alikuwa na wakati mgumu ambao kwa sasa umepita. Anaamini ataanza tena kushambulia mwezi huu, wanahitaji huduma yake.
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top