Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

SIMBA YA MZUNGU YASAFICHA ‘NYOTA’ KOMBE LA MAPINDUZI

SAM_4271KOCHA mpya wa Simba, Goran Kopunovic ameanza vyema kibarua chake Msimbazi baada ya jioni ya leo kuiongoza klabu yake kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar katika mchezo wa kundi C kombe la Mapinduzi 2015.
Bao pekee la Mnyama lilitiwa kambani dakika ya 55 kipindi cha pili kupitia nyota mwenye kipaji cha hali ya juu, Said Hamis Ndemla.
Ndemla  alitia gozi kambani kwa shuti kali nje ya 18 kufuatia pasi murua aliyotengenewa na beki wa kulia Hassan Ramadhani Kessy.
SAM_4231
Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic
Ushindi huo ni faraja kwa mashabiki na wapenzi wa Simba kwani mechi ya kwanza walitandikwa 1-0 na Mtibwa Sugar fc.
Katika mchezo wa leo, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu alihuduhuria na kukunwa na matokeo waliyopata.
SAM_4246
Kikosi cha Simba kilichoanza
Hata hivyo, kocha mkuu alionekana kutoridhishwa na kiwango cha timu na alitumia muda mwingi kuwaelekeza wachezaji wake nini cha kufanya.
Kocha Goran aliwaanzisha Hassan Kessy, Mohamed Hussein ‘Tshabala’, Hassan Isihaka na Abdi Banda katika safu ya ulinzi.
Jonas Mkude alicheza kiungo wa ulinzi wakati winga ya kulia alianza Ramadhan Singano ‘Messi’, winga ya kushoto Awadh Juma na washambuliaji wa kati walianza Danny Sserunkuma na Elius Maguli.
SAM_4244Kikosi cha Mafunzo
Michuano hiyo itandelea kesho kwa mechi nne kupigwa ambapo mabingwa watetezi KCC ya Uganda watachuana na Mtende katika uwanja wa Amaan kuanzia majira ya saa 9:00 alasiri.
Mechi ya pili itaanza majira ya saa 11:00 katika uwanja huo huo ambapo Yanga wataoneshana kazi na Polisi na baadaye usiku saa 2:00 Azam fc watapepetana na KMKM.
Mechi nyingine itapigwa katika uwanja wa Mao dze Tung kwa kuwakutanisha Taifa ya Jang’ombe na Shaba.
Credit: Shaffih Dauda
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top