Hip
hop ni maisha ya watu ambao wanaishi katika misingi fulani ya maisha. Kila
tunachokifanya katika maisha ni misingi ya Hip Hop. Ameyaongelea hayo Nash MC
wakati akihojiwa na kituo cha redio cha E FM hapa Dar es salaam.
Nash
MC ameonekana kuchukizwa sana na watangazaji ambao wanapotosha misingi ya Hip
Hop pia kutopendelea kuzicheza nyimbo za mtindo huu kwani DJs wengi hupendelea
kucheza ngoma wazipendazo tu na zinazovuma sana kwa wakati huo bila kujua kuwa
Hip Hop ni moja tu na wala haibadiliki tofauti na Bongo Flava ambayo hubadilika
badilika.
“Hata
ukienda German utakuta Hip Hop ile ile isipokuwa lugha tu, Ufaransa pia
wataimba kwa Kifaransa Hip Hop ile ile”, alisisitiza.
Pia
ameongelea kuhusiana na serikali kukosa mapato kutokana na kazi za wasanii,
alisema, “Mimi nimeshawahi kutengeneza mixtape yangu na nikaiuza nikapata pesa
nzuri lakini sikulipia kodi, na hakuna mtu aliyenifuata kuulizia suala lolote
la kodi kutokana na kazi yangu”. Hata hivyo alisisitiza kuwa serikali ndo yenye
makosa kwani ingeweza kuirasmisha sanaa na kuweza kuwatoza kodi wasanii, pesa ingepatikana
nzuri. Kungekuwepo na TIN maalumu kwa wasanii na wangekuwa wanalipia kodi
kubwa. Ametoa mfano Marekani kuna wasanii wengi utawasikia au kuwasoma
mitandaoni kuwa wanadaiwa kodi kiasi Fulani tofauti na hapa kwetu Bongo.
SUALA
LA SHOW ZAKE PIA KIPATO
Kuhusiana
na maslahi anayopata, amesema kuwa show moja anaweza kupata hata milioni mbili
na nusu. Hajazungumzia kiundani suala la kipato chake kwa ujumla.
MADAWA
YA KULEVYA NA HIP HOP
Ameulizwa
swali la kizushi kuwa, wasanii wengi wa Hip Hop wanatumia mihadarati, yaani Hip
Hop inaenda samba samba na Madawa ya kulevya. “Kwanza neno stress lifutike kwa
kisingizio kwamba msanii wa Hip Hop ni lazima atumie madawa ya kulevya ili
kuondoa stress, ni uongo kwani tunawaona wengi tu ambao si wana Hip Hop
wanatumia sana, lakini kutumia madawa ya kulevya ni mtu mwenyewe na si sanaa
anayokuwemo”.
WITO
KWA WANA HIP HOP
Ametoa
wito kwa wana Hip Hop wenzake kuwa waangalie pale wanapokosea na waweze
kuparekebisha. “Wakae na kujiuliza ni
wapi wamekosea…”. Pia ametoa maneno ambayo wana Hip Hop wote wakifuata
watafanikiwa, “Peace, Love, Unity and Happiness”.
NENO
KWA WATANGAZAJI
“Watangazaji wengi huenda wamewekwa kiundugu
undugu tu na hawawezi kudadavua vilivyo kuhusiana na kitu Fulani hasa Hip Hop,
wanacheza miziki ya washikaji wao na kusahau kugonga ngoma zilizoenda
kidato. Mara utawasikia wanasema Hip Hop
hailipi, jamani Hip Hop inalipa. Mimi nawaambia hivi, NO RESEARCH NO RIGHT SAY”