Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

HAWA NI WASANII AMBAO MPAKA SASA WAMESHATANGAZA KUGOMBEA UBUNGE MWAKA HUU

Wasanii wa Tanzania, Safari hii wameamua kugombea Ubunge katika maeneo mbalimbali. Hawa ni baadhi ya wasanii walio amua kugombea mwaka huu 2015
                                                                      Profesa Jay, Mikumi-
Nimeamua kugombea jimbo la Mikumi kwa kuwa ni nyumbani. Wazazi wangu waliishi hapa kwa muda mrefu lakini pia nimekuwa nikiimba siasa sana na sasa nimeona huu ni muda wa kufanya yale niliyokuwa nikiimba kuuhusiana na maendeleo ya taifa.”
                                                                  Dude, Tabora Mjini- 
Nimeanza kufanya maandalizi ya kugombea ubunge nyumbani kwetu Tabora mjini, niko tayari kuchuana na yeyote na sasa niko kwenye maandalizi ikiwemo kuwa karibu na wananchi kwani wananikubali, hivyo nitahakikisha ninapata ushindi.
                                                                         JB, Kinondoni-
Nitajitosa rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge. Nia ninayo, uwezo ninao na sababu pia ninayo, ni muda mwafaka sasa wa kutimiza ndoto yangu ya kuitumikia jamii.”
                                                                Soggy Doggy, Segerea
Soggy Doggy ametangaza kugombea ubunge wa jimbo hilo, jijini Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chadema. Jimbo hilo kwa sasa linashikiliwa Makongoro Mahanga (CCM).
                                                                  Steve Nyerere, Kinondoni
Ukiona chereko chereko ujue mambo yameiva, nitagombea ubunge 2015. Nimejipanga na ninaweza kufanya hivyo, nipo vizuri sana.” Jimbo hilo la Kinondoni liko chini ya Mhe. Idd Azzan (CCM).

                                                           Afande Sele, Morogoro Mjini
Niliumizwa baada ya kusikia kuwa eti katiba ya chama cha Chadema inasema kuwa mwanachama anayekwenda mahakamani kudai haki yake anakuwa amejivua uanachama wake. Kwa chama kama Chadema sikuamini kama kingekuwa na sheria kandamizi kama hiyo ya kuwazuia wanachama wake kwenda mahakamani, ndio maana nimeamua nijiunge na chama kingine ambacho kitakuwa kinamuweka huru mwanachama kudai haki zake.” Jimbo la Morogoro Mjini kwa sasa lipo chini ya Mohamed Aziz Abood (CCM).
                                                                 Dokii, Kilosa Morogoro
Mimi ni msanii pekee naweza kusema ndiyo nimetumika sana kwenye jamii kuliko wasanii wote, kwenye kuelimisha jamii najitolea hata kipindi kile cha madereva wa bodaboda mpaka wakanipa Ubalozi nilikua natetea haki zao, pia nataka kuonyesha kwamba wanawake tunaweza.”
Jimbo la Kilosa liko chini ya Mustafa Mkulo (CCM) ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha kabla ya kujiuzulu.
                                                          King Majuto, Tanga Mjini
Mujibu wa maneno yake anasema lengo kubwa ni kutaka kuinua uchumi wa Tanga pamoja na kutetea haki za wananchi pamoja na rasilimali za Mkoa huo. “Nitarudisha Tanga ya zamani ambayo ilikuwa ikisifika sehemu mbalimbali kutokana na rasilimali zilizopo ambazo kwa sasa zimeshindwa kusimamiwa na kuwanufaisha watu wa Tanga.” alisema Majuto ambaye atakua akichuana na mbunge wa sasa wa Tanga Mjini, Omari Nundu (CCM).
                                                                      Shilole, Igunga
Baada ya Dalali Kafumu anayefuata ni mimi, mimi nadhani napenda jimbo langu na nawapenda wakazi wangu wa Igunga wananiona tangu nakua mpaka sasa hivi, kwa hiyo wanafurahi. Sasa wananiambia ‘sisi hatutaki kumpa mtu mwingine kiti hiki sasa na hivyo wananipa changamoto,” alisema msanii huyo.
Vitu viwili vya kwanza ambavyo nitavifanya nikiingia kwenye lile bunge nikiwa kama msanii, kwanza nitatetea haki za wasanii, cha pili Igunga yangu wapo wakazi wa Igunga vijana wapate kazi, yaani akinamama, wale mama lishe na wengine lazima wawe na kazi zao. Kwahiyo nitawatafutia kazi na nitajenga chuo cha muziki".
                                                                      Kalapina, Kinondoni
Kwanza sasa hivi anaitwa mbunge wa Kinondoni, hivyo nitagombea uchaguzi ujao. “Kuna mambo mengi ambayo nimepanga kuifanyia Kinondoni,’’ anasema kalapina.
                                                                  Mrisho Mpoto, Ubungo
“ Nataka kurudisha heshima, utamaduni na maisha bora kwa watu wa Ubungo.” Jimbo la Ubungo kwa sasa liko chini ya John Mnyika (Chadema).
                                                                           Kingwendu
Mwigizaji Kingwendu, anasema anajiandaa kugombea ubunge mwaka huu 2015.Hata hivyo, Kingwendu hakuweka bayana atagombea jimbo gani wala kupitia chama gani, isipokuwa zaidi anasema kuwa chama ambacho kinapendwa na Watanzania wengi ndicho atatumia tiketi yake.
Kingwendu anasema, “Ninajiandaa kugombea ubunge 2015 kupitia chama ninachoona kinapendwa na Watanzania wengi kwenye jimbo ambalo nitalitaja hapo baadaye wakati utakapofika, bado ninafanya mazungumzo na washauri wangu wa karibu kuhusiana na suala hilo, nadhani nitaliweka wazi muda ukifika.”
                                                                   Juma Chikoka, Ilala.
Msanii wa sanaa ya maigizo na filamu, Chikoka maarufu kwa Chopa Mchopanga au Mzee wa Halmashauri ya Kichwa, Mwaka 2010 aliwahi kuchukua fomu na kujitosa kwenye siasa kwa kugombea ubunge wa Jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini alishindwa kwenye kura za maoni za chama hicho na mbunge wa sasa wa jimbo hilo Mussa Zungu.
Mwaka huu wa 2015, amepanga kujitosa tena na safari hii anasema kuwa kinachomsukuma hadi kuamua kugombea tena ni kutaka kuwawakilisha vijana wenzake katika ngazi ya juu ya uongozi na kupambana na uhaba wa ajira kwa vijana.
Anasema kuwa yeye ni mzoefu katika siasa, kwani alishawahi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni, mhamasishaji wa vijana, pia ni mmoja kati ya waanzilishi wa matawi ya CCM nchini India
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top