Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

PATCHO MWAMBA AKANUSHA TUHUMA ZA KUPIGWA BAADA YA KUFUMANIWA


Mwigizaji na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba amekanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
 
Akiongea na mtandao huu, Patcho amesema picha iiliyozagaa mitandaoni aliipost mwenyewe juzi baada ya kupata aleji ya macho ambapo baadaye ilisambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa kapigwa baada ya fumanizi.
 
"Unajua nina aleji na pombe pamoja na vumbi, nikitumia tu pombe lazima macho yangu yavimbe juzi nilikunywa Windhoek mbili na usiku hali yangu ikabadilika na macho kuvimba, baada ya tukio hilo niliamua kujipiga picha na kuipost katika mtandao wa Instagram na hapo ndipo balaa likazuka" Alisema Patcho

Kwa niaba ya mitandao yote ya kijamii Tanzania na duniani kote, BURUDANIKA BLOG inakuomba radhi kwa usumbufu wote uliotokea, Mr Patcho nadhani hizi ni changamoto tu za maisha hivyo tunatakiwa kuwa makini sana, hatukua na lengo la kukudhalilisha bali ndo jamii ilielewa hivyo. 

"Accept our apologies and sorry for any inconvenience that you have experienced", Bongo Central kwa niaba ya mitandao yote duniani kwa namna moja au nyingine ilijaribu kueneza uvumi huu mbya.
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top