Welcome

    Featured Posts

    BURUDANIKA BLOG - KWA MICHEZO NA BURUDANI ZOTE

    .

Loading...

BABA WA MAYWEATHER AMKEJELI PACQUIAO NA SHAIRI LA USHINDI

Floyd Mayweather katika pozi na baba yake mzazi.
BABA wa bondia Floyd Mayweather ameamua naye kumrushia ‘makonde’ Pacquiao, lakini kwa njia ya mashairi ambapo amesema ameshindwa kwa vile mwalimu wake wa ndondi hajui lolote.
Floyd Sr, ambaye ndiye baba yake Mayweather, amekuwa akipitisha muda wake kutunga mashairi, na amekuwa akifanya jitihada za kutoa kitabu kuhusu umahiri wake huo.
Vipande vya mashairi alivyovitoa baada ya pambano kabambe lililofanyika Jumamosi iliyopita vinasema:
Pambano limefanyika…
Heshima ya Manny imepotea bila kuacha alama.
Wakati mimi na Floyd
Tulipokumbatiana kwa furaha...
Niligeuka kumtazama Freddie usoni akiwa ametahayari.
Nimebadili msimamo wangu
Naweza sasa kuwatazama usoni
Na kusema:
Lazima nikiri mlijaribu mlivyoweza…
Kama tulivyoona hapakuwa na ushindani.
FLOYD ndiye bora zaidi!
Sasa kama nilivyosema hapo mwanzo
Freddie amefikia mwisho wake!
© Copyright BURUDANIKA BLOG
Back To Top